---
type: BookChapter
work_id: '1806'
book_url: https://nasa.misia.sk/books/1837
book_markdown_url: https://nasa.misia.sk/books/1837.md
language: cd
position: 28
canonical_url: https://nasa.misia.sk/book_chapters/5508
markdown_url: https://nasa.misia.sk/book_chapters/5508.md
markdown_source: converted
translations:
  cd: https://nasa.misia.sk/book_chapters/5508.md
---

# Barua Ya Muzunguko Decemba 2020

## Leo maandiko haya yametimia

Tunaishi katika siku za wakati wa mwisho mbele yakurudi kwa Yesu Kristo. Tuna ona na macho yetu na kusikiya na masikio yetu namna unabii wa Biblia ukonatimiya kwa wakati wetu – Ikiwa kuhusu kurudi kwa waisraeli katika inchi yao, Ikiwa kuhusu vita na matetesi ya vita, I kiwa kuhusu mitetemeko ya Dunia, Njaa, na magonjwa.Haya yote yalikuwa yalishaka semewa na BWANA wetu katika (Luka 21). Tuna ishi kwa wakati wa joto kali, mabadiliko ya anga, na masumuko ya maumbile ya kila aina. Kwasababu ya virus mupya ambayo ime julikna kwa jina la “Corona**”**na ime sambaa Duniani pote kilakitu kime badilika na hakita rudi kati hali yake yake halisi tena.

Alama mkuu ya mwisho ya wakati nikurudi kwa watu wa israeli katika inchi yao ya ahadi. *“Maana BWANA atamuhurumiya yakobo atamuchagua israeli tena, naye ata waweka katika inchi yao wenyewe…*” (Isaya 14:1). Maneno haya yametimiya machoni petu. Inchi ya Israeli iliongeza kuweko tangu mwaka ya 1948. Mapatano ya salama ya mashariki yakati ime leta uangalifu mkubwa kama vile yazama. Katika mwaka wa 2020, septemba, umoja wa warabu pamoja na Bahrain Wali weka sahihi mapatano ya usalama pamoja na Israeli, walio jiitiliya “Mapatano ya Abrham,” Kama vile Misri walivyo fanya kwa mwaka wa 1979 na Yordani kwa mwaka wa 1994. Inchi nyingi za ki Isilamu pamoja na nyingine zita fuata hapa karibu upesi. Mapatano ya salama Yamwisho itakayo tokeya katika mashariki ya kati, inatarajiwa kupitia upatanisho kati ya Saudi Arabia na Israeli – mpaka hiyo mapatano inayo semwa ndani ya Danieli 9:27 ndiyo ya mwisho. 

Baada ya hayo mapatano yote pamoja na Israeli, kupitiya mapatano ya sheria kubwa zilizo kubaliwa duniani pote, hiyo patano iliyo onyeshwa na Danieli, itamalizwa katika mwisho. Wakati ile usalama, ambao itakuwa tu usalama ya uongo, itakuwa imefikika, *“…Wakati wasemapo, kuna amni na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa gafla, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba wale hakika hawataokolewa…”* (1 Wathesalonike 5:3). Tuna weza kuona mwendeleo ya usalama ikikamata sura yake katika habari za kila siku.

Unyakuo pamoja na mapatano ya usalama utafanyika karibu wakati moja. Pamoja na unyakuo, Wakati ya neema kwamataifa iko nafikiya mwisho, na myaka saba ya mwisho mbele ya kuanza utawala wa miaka elfu. Wakati wa kwanza wa miaka tatu nasu, Manabii wawili watatokea nakuonekana kulingana na Ufunuo 11, kupitiya hao ndipo kuwekwa muhuri kwawale 144 000 kutoka katika kabila 12 ya Israeli kutafanyika. Katikati ya hiyo myaka saba (7) hiyo agano itavunjika, Ziki kuu itaanza, na Yerusalemu itakanyangwa na mataifa yengine mwezi 42 (Ufunuo 11:2).

Kwa kurudi kwa BWANA Ufufuko wa kwanza utafanyika kwawale walio sinziya katika Kristo (1 Wathesalonika 4:13-18). Ufunuo 20:4-6 unaongeya kuhusu ufufuko ya wale walio toka katika hiyo ziki kuu (ufunuo 7:13-14). Hawa hawana sehemu katika Unyakuo na katika Harusi, Lakini wa takuwa katika utawala wa myaka elfu: *“…Nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa yesu, na kwa ajili ya neno la mungu, na hao wasiyo msujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa haiwakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.**Hiyo ndiyo ufufuko wa kwanza.**Heri, na mtakatifu niyeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza, juu ya hao mauti yapili haina nguvu, bali wa takuwa makuhani wa mungu na wakristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.”* (Ufunuo 20:4-6). Na wengine wote watakuwa na sehemu katika ufufuo wa pili, amboyo tena nihukumu ya mwisho, baada ya myaka elfu. (Ufunuo 20: 11-15)

Hatuitaji kuingilia hizo somo, Lakini tuna weza kuona kwamba mwisho unakaribiya. Tunaitaji waamini wa kweli kuwatayari katika unyakuo (1Wathesalonika 4:13-18). Pamoja na kila kitu kinachofanyika kwasasa, tuna weza kufanya kama vile BWANA wetu alivyo sema: “*Basi mambo hayo ya anzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwakuwa ukombozi wenu umekaribia.”*(Luka 21:28).

Tunaweza kusema mara zaidi kwamba: Leo maandiko hii namengineyo imetimiya mbele ya macho yetu! Katika Mathayo 24:14 BWANA wetu alisema, *“Tena habari njema ya ufalme ita hubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapo kuja.”* Injii ya kweli ya milele ya Yesu Kristo haijawai kuchukuliwa ulimwenguni kama vile ilivyo kwa wakati wetu. Kwa wakati uliyo pita, na hata mbele na zaidi sana tangu uamsho, hapo kume kuwa uamsho za kiroho, Lakini hakuna hata moja ya hizo ambao ilitangaza injili halisi akiwa chini ya upako wa Roho Mtakatifu kama vile mwanzoni, wakati kanisa la agano jipya lilipo anza. Sasa injili inayojaa na mafundiso ya Biblia, kama vile Uungu, Ubatizo wa maji, Meza ya BWANA, inapahswa kuwa kama vile ilivyo kuwa Mwanzoni. Badala ya yote, ina semeka tena ku BWANA wetu na mkombozi*: “Ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizo nenwa na Mungu kwa kinyawa cha Manabi wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.”* (Matendo 3:21)

Kwa wakati wetu, Wainjilisti wengi wame hubiri injili zao wenyewe, Wote waelekea kati mwendeleo waki karsimatic. Ijapokuwa wote walipitiwa na ahadi ya muhimu ambayo ingelipashwa kutimilika mbele ya kurudi kwa Kristo. Kama vile mpango wa Mungu ulivyo anza katika agano jipya na utimilifu wa unabii wa Biblia. Katika Marko 1 tunasoma*: “Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu; kama ilivyo andikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako atakaye itengeneza njia yako* (Malaki 3:1a). *Sikiliza, nisauti ya mtu aliyaye itengenezeni nyikani njia ya BWANA, Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu* (Isaya 40:3). *Yohane alitokea akibatiza nyikani, nakuhubiri ubatizo wa toba liletao ondoleo la dhambi. Wakamwe inchi yote ya uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao*.” (Shahiri la 1-5).

Mutu wa Mungu angeliweza kusema kwawale walioamini ujumbe wake: *“Mimi niliwabatiza kwamaji bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”* (Shahiri la 8). Wakati Yesu alipo onekana, alihubiri akisema: „*Wakati umetimiya na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini injili.”* (shahiri la 15).

Katika mahubiri yake ya kwanza baada ya umwangaji wa Roho Mtakatifu, Petro alinea maneno yafuatayo akiwa chini ya upako na uonsgozi wa Roho mtakatifu: *“Tubuni mkabatizwe kilammoja kwajina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la zambi zenu, nanyi mutapokea kipawa cha roho mtakatifu; kwakuwa ahadi hii nikwa ajili yenu, na kwawatoto wenu, na kwa watu wote waliombali, na kwawote watakaoitwa na BWANA Mungu wetu wamjie*.” (Matendo 2:38-39)

Wakati imetimia. Sasa, kwa mwisho ya wakati wa neema, tuko naishi utimilifu wa unabii wa biblia ulio tabiriwa kwa kanisa, kama vile mwanzoni. Kwa mufano, katika Malaki 4:5 inaandikwa: “*Angalieni nitawapelekea Eliya nabii, Kabla haijakuja siku ile ya BWANA, iliyo kuuna kuogafya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo watoto iwaelekee baba zao…” *

Kupitiya hudma ya Yohana Mbatizaji, mioyo ya wa baba wa agano la kale iligeukiya mioyo ya watoto wa agano jipya (Luka 1:17). Kupitiya hudma ya ndugu Branham, Sehemu yapili ilitimiya:Mioyo ya watoto wa Mungu ilirudishwa kuimani ya baba zao mitume huko mwanzoni: BWANA Yesu alishuhudia hii maahadi ya agano la kale katika Mathayo 17:11: *“Naye akajibu akawaambiya, kweli eliya yuaja, naye atatengeneza yote.”* Nabi malaki alitangaza akiwa chini ya upako wa Roho Mtakatifu, Mwokozi wetu alishuhudiya akiwa chini ya upako wa Roho Mtakatifu, nawale wote walio fundishwa kweli kweli wakiwa chini ya upako wa Roho Mtakatifu, wanaamini ahadi nakuona utimiliu wake.

Mungu alimuita mtumishi wake nyumbani kwa mwaka wa 1965 Desemba, Lakini tangu wakati ule, Ujumbe halisi wa kibibilia aliyo ileta ime chukuliwa ulimwenguni pote kulingana na Utume wa Mungu. Inaweza semeka tena hapa: Aliye wa Mungu husikia maneno ya Mungu (Yohane 8:47). Ingawaje, Mtu anaweza naye kuuliza*: “Ni nani aliye sadiki habari tuliyo ileta ? Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani?”* (Isaya 53:1, Warumi 10:16). 


## Chapter navigation

- [Previous chapter](https://nasa.misia.sk/book_chapters/5507.md)
- [Book contents](https://nasa.misia.sk/books/1837.md)
- [Next chapter](https://nasa.misia.sk/book_chapters/5509.md)

## Available translations

- [Swahili DRC](https://nasa.misia.sk/book_chapters/5508.md)

## Source

- [Canonical HTML page](https://nasa.misia.sk/book_chapters/5508)
- [Markdown representation](https://nasa.misia.sk/book_chapters/5508.md)
