BARUA YA MUZUNGUKO Septemba 2009
Katika Barua yetu ya mwisho ya Waraka, ya Aprili/Mei 2009, tuliandika kuhusu wito na maandalizi ya wale walio wa Kanisa Bibi-arusi. Jibu lilikuwa kubwa sana. Tumegundua jambo muhimu ni leo, yaani utiifu wa imani, maisha ya kiuungu ya Bwana-arusi katika Bibi-arusi. Kama ilivyoelezwa na Ndugu Branham katika mahubiri yake, tumekazia sawasawa: “Katika Wana-kondoo wasiohesabika wa Agano walichinjwa na damu yao ili mwangwa kwa ajili ya upatanisho, lakini uhai wa wanyama waliotolewa dhabihu haungeweza rudi ndani ya wale waliotoa dhabihu. Hata hivyo, kupitia dhabihu ya Mwana wa Mungu, ambaye damu yake ilimwagwa Kalvari kwa ajili ya upatanisho, muujiza wa miujiza yote ulifanyika. Uzima wa kiungu uliokuwa ndani ya Mkombozi inapatika kwa kuzaliwa upya kwa wakombolewa. Wana na binti wote wa Mungu wana maisha yale yale yaliyokuwa katika Mwana wa Mungu, pamoja na fadhila zote, kwa hakika, pamoja na tabiya yenyewe ya Yesu Kristo.”
Ifuatayo ni kweli milele: “Kwa yeye atakasaye na wao pia waliotakaswa wote watoka kwa mmoja; kwa sababu hiyo haoni haya kuwaita ndugu, akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu katikati ya kanisa nitakuimbia sifa … Kwa hiyo katika yote ilimpasa kufananishwa na ndugu zake, ili yeye awe kuhani mkuu mwenye rehema na mwaminifu katika mambo ya Mungu, amfanyeupatanisho kwa ajili ya dhambi za watu.” (Waebrania 2:11-12+17)
Kundi lililonunuliwa kwa damu yake linahesabiwa haki mara moja na kwa milele wote na kutakaswa katika Yeye, “Ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kuwekwa kufufuka tena kwa ajili ya kuhesabiwa haki.” (Warumi 4:25)
Wanaitwa waliobarikiwa tayari katika ulimwengu huu: “… Heri yao ambao maovu yao yamesamehewa, na waliositiriwa dhambi zao. Umebarikiwa mtu ambaye Bwana hatamhesabia dhambi.” (Warumi 4:7-8)
Kwa Roho Mtakatifu wanaongozwa katika kweli yote ya Neno na wanaongozwa kutakaswa humo: “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” (Yohana 17:17)
Pia sehemu yake ni ufunuo wa Jina la Yesu, ambapo Mungu kama Baba ametupa vitu vyote katika Mwanawe: “Nimelidhihirisha jina lako kwa watu ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, nawe ukanipa wao; nao wamelishika neno lako.” (Yohana 17:6)
Kabla ya Bwana kusema katika Agano Jipya, “Amri mpya Nawapa ninyi, kwamba mpendane; kama nilivyowapenda ninyi, nanyipia pendaneni.” (Yohana 13:34), Alisema katika Agano la Kale kwamba Angefanya agano jipya na kuwapa watu wake moyo mpya, roho mpya, hata maisha mapya (Yeremiya 31:31-34; Ezekiel 18:31-32; a. o.).
Ukombozi ni mkamilifu kadiri uwezavyo kuwa: kuhesabiwa haki kamili, kufanywa upya, na kuzaliwa upya kwa uwezo wa kufufuka kwake Yesu Kristo kutoka kwa wafu, njia yote ya kujazwa, kutiwa muhuri, na kuongozwa na Roho Mtakatifu.