Circular Letter
Barua ya muzunguko - Juni 1973
Ewald Frank
Navigate
Kapitel
expand_more
Navigate
Kapitel
Navigate
Kapitel
Jump to any chapter without leaving the reader.
Kapitel 2
UONGOZI WA ROHO NI NINI?
2 / 6
“Kwakuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana waMungu.” (Rum. 8:14) Kwa vitendo, uongozi wa Roho unamaanishakwamba tutambue kile ambacho ni sawa machoni pa Mungu, kwamba tunakiweka kwa matendo, na kwamba kinaonyeshwa kwa wakati unaofaa. Tunapatamfano wazi wa hilo katika Luka 2:25-32. Simeoni alikuwa amepokeaufunuo wa ahadi ya Neno kwa wakati wake, naye akaongozwa na Roho Mtakatifu ndani hekalu: nihapo ambapo aliona kwa macho yake mwenyewe utimilifu wa Neno. Chini yaupako wa Roho, akatmka unabii huu wa ajabu kuhusuYesu.
Tunaona hapa ni nini uongozi wa Roho wa kweli naya kibiblia. Sio utawa ya kujipendeza, lakini ukweli nikutambua ufunuo wa mapenzi ya Mungu na ahadi zake ambayo kwa hiyo huongozwakwawakati unaofaa namahalipazuri ili kuwa shahidi kuhusu kile Mungu anachofanya. Roho Mtakatifu hatufanyi sisi kupita pembeni yaKristo na ahadi zake. Wote ambao wanaongozwa na Roho wa Mungu wanatambua pia kwa siku zetuutimilifu wa maahadi. Wanakuja kwa Yesu na, wakisukumwana Roho Mtakatifu, wanatangaza kile ambacho kina timilika kulingana naNeno la Mungu. Nao pia, wakiongozwa na Roho wa Mungu wanatambua kazi ya Mungu na kuishiriki.
Kwa kipekee kwenye nafasi za „Injili Kamili“, kunasikilika sana kuhusu uongozi wa Roho Mtakatifu; lakini sisi lazima daima kuchungambele ya macho yetu wazo hili ambalo Roho Mtakatifu anaongoza katika kweli yote. Mutu ambaye kweli kweli anaongozwa na Roho wa Mungu anasema hiyo kwa shida. Yeye hapige tarumbeta mbele yake, lakini popote aendapo huacha alama za baraka. Kuna kitu cha muhimundani yake. Yeye si mupendelevu, wala mutu wamipaka. Hapana, katika uepo yake, kila mtu anajisikia vizuri. Mwenendo wa mtu wa namna hii una elezewa katika Neno kwa maneno haya: “… uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.” (Wakolosai. 3:3) Ingawa hivyo maisha yake yanafichwa ndani ya Mungu, mishale ya uzima huo haifichwi, yeye, kwa sababu: „Kristo, uhai wenu; atakapo funuliwa nanyi pia mutafunuliwa pamoja naye katika utukufu” (Wakolosai. 3:4).
Watu wa kweli wa Mungu hawa semi kwa ajili yao wenyewe, na ushuhuda wao hauhusiani na "umimi" wao. Hawawekikwa sehemu ya kwanza mazoezi yao ili wajitukuze, lakini, wanautukuza utukufu wa Bwana, Mungu wao. Ikiwa tunataka kuonekanapamoja na Kristokatikautukufu, lazima tayari adhihirishwe hapa ndani ya maisha yetu. Mungu alifichwa ndani ya Kristo, hata hivyo, kazi za Munguzilidhihirishwa kupitia Yeye. Vivyo hivyo, Kristo, uzima wetu, amefichwa ndani yetu; kwa hivyo, kazi Zake zitadhihirishwa ndani yetu.
“… wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu…” Katika Agano la Kale na Agano Jipya, tunayo mifano ya kutosha ya watu walio puliziwa na kuongozwa na Roho wa Mungu. Yesu Kristo, Bwana wetu, anatuonyesha alama yauhakika ya utendaji wa Roho Mtakatifu: “…atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu … yeye atawaongoza awatie katika kweli yote … atanena yote aliyo yasikia, na atawaambia mambo yajayo. Atanitukuza, kwa sababu atachukua yaliyo yangu, naye ataiwatangazia…” (Yohana 16:8-14) Ni hayo yote ambayo Roho Mtakatifuanazihirisha katika maisha ya mtu anayekuja kwa Kristo na kupokea neema yake. Anaanza kwa kumwongoza kwenye maungamo ya dhambi zake, kwa toba, kwa matengenezo ya makosa yake, na kukubalishwa, kwa kuzaliwa upya, kwa kusafishwa na utakaso, tena kwakumaliza, humjaza Roho Mtakatifu. Mahali kitendo hiki na alama hizi za wazi vinakosa nikusema kwamba kitu fulani si katikautaratibu.
Available translations
PDF
EPUB